Isaiah 66:3

3 aLakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali
ni kama yeye auaye mtu,
na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,
ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.
Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,
ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,
na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,
ni kama yule aabuduye sanamu.
Wamejichagulia njia zao wenyewe,
nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.
Copyright information for SwhNEN